LVIV, UKRAINE
MARIO Balotelli juzi Jumapili alibaguliwa kwa kupigiwa kelele za nyani na mashabiki wa Hispania wakati wa pambano la Euro 2012 la hatua za makundi kati ya Italia na Hispania. Hata hivyo hakutoka nje.
Hilo lilikuwa tukio la tatu la ubaguzi wa rangi baada ya kusemekana kuwa wachezaji weusi wa timu ya taifa ya Uholanzi walibaguliwa wakiwa mazoezini, kabla ya beki mweusi wa Czech,Thedor Gebra Selassie, kubaguliwa uwanjani.
Balotelli, ambaye alicheza ovyo katika kipindi cha kwanza cha pambano hilo kabla ya kutolewa, awali alikuwa ametishia angeondoka uwanjani wakati wa mechi kama angebaguliwa.
Mpiga picha Chris Brunskill, kutoka Jiji la Liverpool, alishuhudia tukio hilo wakati pambano hilo likiendelea katika Uwanja wa Arena Gdansk wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 40,000
�Nilikuwa nimekaa nyuma ya lango na mashabiki wa Hispania na walikuwa wanapiga kelele za nyani pamoja na vicheko vyao.
Ilitokea kila Balotelli aliposhika mpira. Alisema Brunskill.
�Wapiga kelele wawili walikuwa wamevaa mavazi kama anayovaa mcheza tenisi wa Hispania, Rafa Nadal. Lakini walinzi wa uwanja walikuwa wanadhani ni vicheko vya kawaida na hawakufanya kitu. Walidhani yalikuwa masikhara.
�Hawa wawili walikuwa katikati ya kundi kubwa la mashabiki wa Hispania. Naweza kusema kulikuwa na mashabiki kama 200 hadi 300 waliowaunga mkono.
�Ilikuwa mbaya wakati Balotelli alipokuwa anajihusisha na matatizo ya uwanja. Kwa mfano pale alipopewa kadi ya njano.
Wakati huo huo, Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje ya Uingereza, amewapa ushauri wachezaji wa England kuondoka uwanjani kama watabaguliwa katika mechi zao za Euro 2012.
�Naunga mkono kwa waamuzi kuchukua hatua kali dhidi ya wabaguzi kutoka majukwaani. Wana nguvu ya kusimamisha mechi. Hata hivyo, kama wachezaji wa England na menejimenti wakiona kuna haja ya kutoka nje wanaweza kufanya hivyo.
0 Comments