Idadi ya watu wanaokimbilia kwenye kambi ya wakimbizi ya Dadaab imeongezeka na
kufikia watu laki nne na elfu sitini na tano. Mashirika yanayotoa misaada
yameonya kuwa kati ya idadi hiyo, takriban watu laki moja na elfu thalathini
watakosa makaazi hivi karibuni na kuishi katika mazingira magumu ndani ya hema
zisizoweza kuhimili dhoruba ya upepo na mvua.
Mashirika yameonya kuwa kuanzia mwezi septemba kutakuwa na upungufu wa maji na vyoo halikadhalika huduma za afya. Kwa wakati huu wahudumu wa afya wamezidiwa na idadi kubwa ya watu -mfano uliopo wa vituo viwili vya afya katika kambi ya Hagadera inayohudumia wakimbizi 78,000.
Wakati vyombo vya habari vikizingatia kuwa kiwango cha wakimbizi wanaoingia kambini kinaliongana na mchango wa pesa zilizochangishwa, mtazamo umegeuka na wahisani kubadili maoni yao kuelekea kwingine kama janga la ukame uliolikumba eneo la Sahel.

0 Comments