Kazi ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya inaendelea katika mikoa minane ya Tanzania Bara na Zanzibar. Wananchi wa rika na jinsia mbalimbali wanajitokeza kutoa maoni yao ambayo ni muhimu katika mchakato huu. Picha hizi ni kutoka Pwani, Pemba, Shinyanga, Tanga.Mwenyekiti wa Mtaa wa Mjini, kata ya Kishapu Mjini, Wilaya ya Kishapu, Bw. Tido Nuhu (52) akiwakaribisha Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya uliofanyika kijijini hapo.
Bi. Faida Faki Kombo wa Shehia ya Makombeni, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano uliofanyika Makombeni leo.
Bi. Siwema Shabaan Mbato, mkazi wa kijiji cha Bwilingu, Tarafa ya Msoga, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano uliofanyika kijini hapo.
Baadhi ya wakaazi wa kijiji cha Bwilingu, Tarafa ya Msoga, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wakisoma kitabu kinaelezea katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lugha nyepesi. Wakazi hao walihudhuria mkutano wa kukusanya maoni yao kuhusu Katiba Mpya uliotishwa na Tume kijijini hapo
Bi. Aziza Juma (27), mkazi wa Wilaya ya Kishapu, mkaoni Shinyanga akitoa akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipofanya mkutano kijijini hapo.
Wananchi wa Kijiji cha Maganzo, Kata ya Songwa, Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wakifuatilia mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya jana
Bi. Scholastica Benard, mkaazi wa Kata ya Minziro, Wilaya ya Misenyi, mkoani Kagera akitoa maoni yake kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipofanya mkutano wake wilayani hapo .
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba katika picha ya kumbukumbu na wanafunzi wa Shule ya Msingi Michungwani iliyopo kijiji cha michungwani, Kata ya Segera wilayani Handeni mkoani Tanga mara baada ya mkutano wa kukusanya maoni kuhusu Katiba Mpya.
1 Comments
My web site - planning a wedding on a budget