Watu wapatao 35 wamekufa kufuatia mafuriko yaliyotokea katikati
mwa Nigeria baada ya mvua kubwa na kusababisha bwawa kufurika karibu na mji wa
Jos.
Msemaji wa shirika la msalaba mwekundu katika eneo hilo amesema nyumba zipatazo mia mbili, nyingi zikiwa zimejengwa kwa udongo zimezama au kuharibiwa na mafuriko.
Maafisa wanasema watu wapatao ishirini na watano hawajulikani walipo na kwamba idadi ya watu waliokufa inatarajiwa kuongezeka.
Shirika la Taifa la Kushughulikia Majanga limeanza operesheni ya misaada ya dharura.
Mtu mmoja alinukuliwa akisema kuwa amewapoteza watoto wake saba katika mkasa huo.
Msemaji wa shirika la msalaba mwekundu katika Jimbo la Plateau amesema miongoni mwa waliofariki ni mzee wa miaka 90.
0 Comments