Wanaharakati wa haki za wanawake nchini Ivory Coast, wamepongeza hukumu ya
kifungo jela iliyotolewa kwa mangariba tisa au wanawake wanaopasha tohara kwa
kitendo cha kuwapasha tohara wasichana wadogo.
Kitendo hicho kimeharamishwa nchini Ivory Coast kwa miaka kumi na minne
sasa.
Lakini ni mara ya kwanza kwa mtu yeyote kuhukumiwa kwa kitendo cha upashaji
tohara.
Mwanaharakati mashuhuri wa kutetea haki za wanawake, Constance Yai, ammesema
uamuzi huo huenda ukawapa motisha majaji wengine kutoa hukumu sawa na hiyo
kuhusiana na visa vya upashaji tohara.
Utafiti uliofanywa ulionyesha kuwa zaidi ya theluthi moja ya wanawake wote
nchini Ivory Coast wamepashwa tohara licha ya miradi mingi tu ya kuhamasisha
watu dhidi ya upashaji tohara.
0 Comments