Rais Jakaya Mrisho Kikwete akuhutubia katika mkutano wa kimataifa wa viongozi kujadili Uzazi wa Mpango kwa nchi masikini zaidi duniani, katika ukumbi wa Queen Elizabeth II jijini London July 11, 2012. Mkutano huo ni wa kwanza wa aina yake duniani na umeanzisha Mchakato wa Dunia ambao utalenga kuwawezesha wanawake wapatao milioni 120 katika nchi masikini zaidi duniani kupata habari, huduma na mahitaji ya kupanga uzazi bora zaidi na kuokoa maisha yao ifikapo mwaka 2020.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa British Gas (BG Group), Sir Frank Chapman (wa pili kulia) na maafisa waandamizi wa kampuni hiyo. BG Group imewekeza kiasi cha Pauni 80 za Uingereza (Shilingi Trilioni 125) katika mradi wa kuchimba gesi asilia nchini Tanzania, na tayari visima vitano vya nishati hiyo vimeshatema gesi nyingi katika bahari kuu kusini mwa Tanzania maeneo ya Mtwara. Hii ilikuwa ni ziara fupi katika makao makuu ya BG Group mjini Reading, Uingereza ambako Rais Kikwete na ujumbe wake walitembelea Julai 11 kujionea namna kazi za uvumbuzi wa gesi asilia unavyofanywa na kampuni hiyo yenye kufanya shughuli zake katika nchi 21 katika mabara matano, ikiwa na jumla ya wafanyakazi 6,000.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. Donald Cameron, Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakijiandaa kupanda jukwaani kuhutubia katika mkutano wa kimataifa wa viongozi kujadili Uzazi wa Mpango kwa nchi masikini zaidi duniani. katika ukumbi wa Queen Elizabeth II jijini London July 11, 2012. Mkutano huo ni wa kwanza wa aina yake duniani na umeanzisha Mchakato wa Dunia ambao utalenga kuwawezesha wanawake wapatao milioni 120 katika nchi masikini zaidi duniani kupata habari, huduma na mahitaji ya kupanga uzazi bora zaidi na kuokoa maisha yao ifikapo mwaka 2020.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu wa British Gas (BG Group), Sir Frank Chapman alipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo mjini Reading Uingereza Julai 11, 2012. BG Group imewekeza kiasi cha Pauni 80 za Uingereza (Shilingi Trilioni 125) katika mradi wa kuchimba gesi asilia nchini Tanzania, na tayari visima vitano vya nishati hiyo vimeshatema gesi nyingi katika bahari kuu kusini mwa Tanzania maeneo ya Mtwara. Hii ilikuwa ni ziara fupi katika makao makuu ya BG Group mjini Reading, Uingereza ambako Rais Kikwete na ujumbe wake walitembelea Julai 11 kujionea namna kazi za uvumbuzi wa gesi asilia unavyofanywa na kampuni hiyo yenye kufanya shughuli zake katika nchi 21 katika mabara matano, ikiwa na jumla ya wafanyakazi 6,000.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mdogo wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza Bw. Stephen O'Brien jijini London, ambapo Uingereza iliahidi kuendelea kuisaidia Tanzania katika mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kusaidia kuendeleza sekta ya nishati hususan utafutaji wa gesi asilia.





0 Comments