Nd.magangaone.
      Napenda kukupongeza kwanza kwa jitihada na kazi yako unayoifanya kupitia kwenye blog yako (welldone).
   
      Mimi ni mmoja kati ya watu wanaoitembelea blog yako, Na ninathubutu kusema ni moja kati yazile best.

      Lakini mimi ninatofautian na wewe katika hili suala la MUUNGANO.

        Kwanini nasema hivyo, Wewe unaonekana ni muumini (pro) wa muungano, Kama hivyo ni sawa, basi

     hapa ndipo tunapotofautiana (baina ya mimi na wewe).  Kama unavyofahamu katika misingi mikubwa ya

    haki za binaadam, moja ni demokrasia. Hivyo hata kama mtu mtakua mnatofautiana kimtazamo, bado

   unapaswa kuheshimu msimamo wake. mimi ninaheshimu msimamo wako.

      Ningependa kukueleza kwamba, Jambo lolote la Umoja huwa ni zuri,Kwani hata vitabu vyote vya dini

   vinahimiza umoja na usawa.  hata ndoa ni moja kati ya umoja, ndio maana alieoa na asieoa hawawi  sawa.

   Kwamsingi huo basi Umoja ni mzuri.

     Sasa tuutizame huu muungano wetu. Namimi napenda kujikita upande mmoja wa muungano: ZANZIBAR.

    Zanzibar imefanya mapinduzi tarehe 12-1-64. Nini malengo ya mapinduzi. Moja kubwa ni kutaka

   Wazanzibari wajitawale(wawe huru,kufanya na kujiamulia mambo yao). Jee! hili lipo kwa sasa??

    Huu muungano wenyewe ulianzishwa bila ya ridhaa ya wananchi. Sasa hiyo demokrasia iko wapi??

   Kama unavyojua serikali ya mapinduzi ya zanzibar imeingia madarakani baada ya mapinduzi ya 1964,

    Hivyo serikali hiyo ndio ilioleta muungano huu. Jee ikiwa serikali yenyewe ilikosa uhalali(legitimacy),

   Jee! huu muungano utakua vipi??. Huu muungano wenyewe unamasuala tele ambayo hayana jawabu

  Kama alivyoyaoredhesha Mh. Othman (mwnasheria mkuu wa zanzibar),na hata Mhadhiri mkuu wa

   kitengo cha sheria aliestaafu wa chuo kikuu cha dar es salaam Prof. Issa Shivji alithibitisha hilo.

        Muungano huu unalindwa kwa gharama yeyote ile na upande mmoja wake,wakati huku

    upande wapili washachoshwa.   Sasa ukitaka wewe ukione ilikuwa uudadisi au uje na maoni tofauti

   na ya bwana.       Alianza mzee karume, baada ya kuona mambo yanakwenda vyengine. akataka

    mambo tele yabadilishwe, nini kilimkuta kauwawa (1972).    Mama Fatma karume(mjane wa karume)

    hivi majuzi tu alijitokeza hadharani aksema huu sio muungano aloutaka mumewangu, na haya

    angekuwapo asingeyakubali.   Mzee Aboud Jumbe nae, alipotaka bora ziwe serikali tatu.

    Akaambiwa ajiuzulu, tena chini ya ulinzi mkali.   Sasa jiulize Rais jumbe ni rais wa Zanzibar

    ambae amechaguliwa kwa kura na wazanzibar, Jee! inakuaje auzuliwe kwa nguvu na bwana

   mkubwa Dodoma.  Wapo wengine wengi ambao yamewakuta, akiwemo Ramadhan a shaaban

   na hata Maalim seif sherrif hamad. Sasa jee! kwanini bara wanafanya hivi??

      Sasa lile alolitaka Mh.Jumbe, Ramadhan shaaban na Maalim Seif Sherrif  wakati ule, ndio hili

    ambalo linafanyika sasa hivi(marekebisho ya katiba). Lakini sasa dunia imebadilika hizi sasa ni
  
    zama nyengine.   Nini wazanzibar wanataka sasa:  Kwanza nchi yao yenye hadhi yakuitwa nchi,

    yenye mamlaka kamili na nguvu zake zote kama dola. ikiwapo uanachama wake UN. Halafu tena

   watu waulizwe kupitia kura ya maoni, Jee wanataka muungano au la, kama ndio mfumo upi

   Muungano wa serikali ngapi; 1,2 au tatu. Au wanataka muungano wa mkataba tu (shirikisho)

   Kama ule wanchi za ulaya.  Sasa kukurupuka tu kwa rais Kikwete na kutaka wananchi watoe

   maoni kuhusu katiba mpya sio dawa. Hii ni janja ya nyani tu.  

    Sio muamsho, sio watu wa kawaida Wazanzibari hawataki tena. Na hili ndio wanaololiogopa

  serikali ya bara. lakini hili ni kama jipu na limeisha wiva.

    Muungano wa kijamii baina ya watu wa bara na zanzibar upo kabla hata ya huu muungano

 waserkali(big brother na small brother). Haya hayataondoka tumekwisha changanya damu.

  Ireland ilkuwa Kwenye muungano na UK kwa muda wa miaka 1800, baadae waliamua kujitoa

 na mpaka leo wanashirikiana wananchi wake. Uliovunjika ni Muungano wa kiserikali sio wakijamii.

    Hii ni karne ya 21, vijana tunasoma na tunafuatilia mambo, kwani tuna university tano Zanzibar.

    Hivyo rais Kikwete asijidanganye sio muamsho ila Uprising kama alivyoona Egypt,Algeria na syria

    hayo zanzibar hayaipukiki, hasa wakati huu ambao wazanzibari washamjua mbaya wao.

    Si ccm wala cuf, vyama baadae kama walivyossema wawakilishi (Hamza,Raza,Jussa,Mansour nk)

     Sasa zanzibar kwanza(FIRST ZANZIBAR). Hiyo ndio slogan ya wazanzibari.   na hasa wakati huu

    wa maombolezi ya ajali ya meli na mfungo wa ramdhan, na ndio kwanza askari wa jeshi la muungano

     wanawapiga watu mabomu, ijumaa tena msikitini na ramadhani hii.    Ama kweli huu sio muungano

   ni utawala wa Kikatoliki.    Kama huyo mpenzi wenu baba wa taifa la Tanganyika Nyrere alivyowahi

    kusema" muhindi yule alikuwa anasema serikali yote ya TZ ipo mfukoni mwake, niliposikia nikamtia

  ndani, wakaja watu chungunzima kuanzia familia yake, hata viongozi mbalimbali sikumtoa. lakini

    ulikuja ujumbe wa papa Bernedict kutoka vertican, hapo ndipo nilimtoa nasikia hata afrika ya mashariki

    anaogopa kuja sasa hivi muhindi huyo".     Huu si muungano bali Wazanzibari wanatawaliwa.

        Lakini naona mambo yameisha. Kabla ya hata uchaguzi ujao hapa Zanzibar will be free.
  PS:  ukitaka majina ya vitabu kuthibitisha kuwa Muungano huu sio halali kisheria nambie nitakutajia,
          ili utafute uvisome. 
  
Magangaone blog is the best

       22/7/2012