Serikali ya Uholanzi imesitisha msaada wa dola milioni 6.15 kwa
Rwanda baada ya nchi hiyo kuhusishwa na ufadhili wa waasi katika Jamuhuri ya
kjidemokrasia ya Congo.
Hatua hii inajiri siku kadhaa baada ya Marekani kutangza inanuia kupunguza
msaada wa kijeshi kwa Rwanda.
Hata hivyo Rwanda imekuwa ikikanusha madai ya umoja wa mataifa kuwa
inafadhili kundi la waasi wa M23 mashariki mwa DR Congo.
Waasi hao walianza kutoka jeshini kuanzia mwezi Aprili na hadi kufikia sasa
takriban watu 200,000 wametoroka makwao kwa sababu ya mapigano kati ya jeshi na
waasi hao.
Hatua hii ya Udachi inajiri baada ya afisaa mkuu wa umoja wa mataifa kuambia
BBC kuwa wanajeshi wanaotoka katika jeshi la DRC wamekiri kusajiliwa na
Rwanda.
Mnamo siku ya Alhamisi, Umoja wa mataifa uliripoti kuwa wana
jeshi wake walisaidia jeshi la DRC kuwafukuza waasi hao kutoka mji wa Goma
kwa kutumia helikopta pamoja na magari ya kijeshi.
Mfumo wa sheria.
Mwandishi wa BBC mjii Hague, Anna Holigan, anasema kuwa hii ndio hatia ya
kwanza ya kifedha kuwa rais Kagame huenda ameanza kuwapoteza washirika wake wa
Ulaya.
Waziri wa mambo ya nje wa Uholanzi, amethibitisha kuwa kuanzia sasa
haitafadhili vyovyote serikali ya Rwanda hadi pale itakapoweza kuhakikishiwa na
Rwanda kuhusiana na madai hayo.
Pesa hizo ilizokuwa inapokea Rwanda zilikuwa zinatumika kuinia hadhi ya mfumo
wa sheria wa Rwanda, ingawa mashirika yasiyo ya kiserikali yataendelea
kufadhiliwa.
Serikali ya Udachi hata hivyo ingali inasubiri jibu kutoka kwa Rwanda
kuhusiana na hatua hiyo wakati ikiendelea kushauriana na nchi zingine za Ulaya
kuhusu hatua zaidi dhidi ya Rwanda. |
0 Comments