Rais wa zamani wa Tunisia Zine el-Abidine Ben Ali amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kuhusika katika mauaji ya waandamanaji wakati wa uasi nchini humo mwaka uliopita.
Kiongozi huyo Ben Ali ameshtakiwa kwa kuhusika kwake moja kwa moja na vifo vya waandamanaji 43.
Zaidi ya watu 300 waliuwawa kwa pamoja katika maandamano ya uasi wa umma nchini Tunisia ambao hatimaye yalisababisha rais huyo kung’olewa madarakani.