Muigizaji nguli wa filamu wa Bara Hindi Rajesh Khanna amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 69.
Kwa mujibu wa taarifa iliyokaririwa kutoka katika familia yake ni kuwa amekuwa akisumbuliwa na maradhi mara kwa mara japokuwa chanzo cha kuugua kwake hakijulikani.
Rajesh Khanna alijijengea jina katika ulimwengu wa filamu za kihindi baada ya kucheza filamu kadhaa za mapenzi zilizovuma miaka ya 1960 na 1970.
Khanna alimeigiza katika filamu zaidi ya 160 zikiwemo zilizopata umaarufu kama vile Kati Patang, Aaradhana, Anand na Amar Prem.