Timu ya Yanga SC ya jijini Dar es Salaam jana imefanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya Kombe la Kagame baada ya kuitoa timu ya Mafunzo kutoka Zanzibar kwa jumla ya penalti 5 kwa 3. Mpaka mwisho wa dakika 90 matokeo yalikuwa 1-1 na ndipo zilipoamriwa zipigwe penalti. Penalti za Yanga zimefungwa na Said Bahanunzi, Nadir Haroub, Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima na Athuman Idd.
0 Comments