Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaa leo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Al Madina, Sheikh Ally Mubaraka alisema hayo wakati alipokuwa akipata futari kwa pamoja na waislamu wa Msikiti wa Sheikh Gorogosi, Tandika kwa Maguruwe.
Alisema fedha hizo zimepatika kutokana na ushirikiano mzuri uliyopo kati ya Ubalozi wa Emirate na taasisi hiyo inayojihusisha na utoaji misaada katika jamii yenye mahitaji maalum.
Sheikh Mubaraka alisema taasisi hiyo inalenga kutoa futari kwenye makundi ya watu ikiwa ni ishara ya huruma kama dini hiyo inavyoelekeza.
“Ubalozi wa Emirate umejitolea fedha za kutosha kwa ajili kufuturisha ambapo leo (jana), tumeanzia Tandika, mpango huu ni wa kila mwaka na utafika katika maeneo yote ya mkoa wa Dar es Salaam”alisema Sheikh Mubaraka.
Sheikh Mubaraka aliwaasa wafanyabiashara kuacha kupandisha bei za bidhaa kwa ajili ya kujipatia kipato kikubwa ambapo sheria za dini zinawataka wanadamu kuoneana huruma wakati wote.
Vilevile alisema mwezi huu wa mfungo Ramadhani ni fursa njema ya kufanya ibada kitendo ambacho kitawasidia waislam kufutiwa dhambi zao.
“Yule mwenye kula mchana katika mfungo huu,hata kama atakuwa akijibidiisha na swala atambuwe kuwa hatoweza kufutiwa dhambi zake”alisema Sheikh Mubaraka.
Akizungumzia tukio la kuzama kwa meli ya Skagit, alisema taasisi hiyo imetoa pole kwa familia zote zilizopoteza ndugu zao kwani tukio lile ni kubwa ambapo uchungu wake umemgusa kila mtu katika nchi hii.

0 Comments