Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu wa Zanzibar, Hamad Masoud
amejiuzulu kufuatia shinikizo za za watu na maandamano.
![]() |
Waliokufa katika ajali ya MV Skagit
|
Kumekuwa na msukumo kutoka kwa makundi mbali mbali ya kutaka waziri huyo
ang'atuke kufuatia kuongezeka kwa ajali za baharini katika Hatua hii imekuja
kufuatia madai ya wananchi kuwa ajali za meli zimekuwa zikiongezeka mjini
Zanzibar bila yeye kuchukua hatua yeyote.
Mbali na kujiuzulu kwa Hamad kama Waziri, Rais wa Zanzibar Ali Mohammed Shein
ameunda Tume ya kuchunguza kiiini cha Meli hiyo ya MV Skagit kuzama na kuuwa
watu.
Mwenyekiti wa tume hiyo atakuwa Jaji Abdulhakim Ameir Issa, wanachama
watakuwa Meja Jenerali S.S. Omar, Komanda Hassan Mussa Mzee, Kapteni Abdulla
Yussuf Jumbe, Kaptein Abdulla Juma Abdulla, Salum Taoufiq,Kaptein Hatibu
Katandula, Bi. Mkali Fauster Ngowo, Ali Omar Chengo na Shaaban Ramadhan Abdalla
Katibu wa Tume.
Kufuatia shinikizo hizo Siku ya Ijumaa ,tarehe 20 Julai ,Hamad Masoud
alimuandikia barua rais wa Zanzibar kumuomba kujiuzu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka chama tawala cha CCM, Rais wa Zanzibar Ali
Mohammed Shein amekubali ombi la Waziri Hamad Masoud kujiuzulu.
Kufuatia kujiuzulu kwa waziri huyo, Rais ,Dk Shein amemteua Mbunge wa Jimbo
la Ziwani Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri mpya wa Miundombinu na
Mawasiliano.
Taarifa kutoka ikulu zinasemna kuwa uteuzi wa Bwana Rashid Seif Suleimna
utaanza mara moja.
0 Comments