Uingereza inaunga mkono mpango wa nchi za Ulaya-EU kuiondolea vikwazo Zimbabwe ili kushawishi uchaguzi huru na wa haki, waziri anayehusika na masuala ya Afrika amesema.
Waziri huyo Henry Bellingham amesema kusitisha vikwazo kwa masharti itakuwa ni hatua kubwa muhimu.
Na itategemea na kuwepo kura ya maoni juu ya mabadiliko kufanyika kabla ya uchaguzi.
Mawaziri wa nchi za Ulaya wanakutana Jumatatu kuamua iwapo kuondoa vikwazo kupitia fedha za msaada moja kwa moja kwa serikali ya Zimbabwe, vibali vya kusafiria na mali.
Bwana Bellingham amesema Uingereza iko makini kusaidia mipango ya nchi za Jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika-SADC kupunguzia mzigo Zimbabwe.