Raia mmoja kutoka Lithuania jijini London amehukumiwa adhabu ya kulipa faini ya pauni za Uingereza 2500 kwa kosa la kejeli za ubaguzi wa rangi katika michezo ya Olympic jijini London.

Petras Lescinskas mwenye umri wa miaka 36 mhasibu kitaaluma, alishtakiwa kwa kutenda kosa hilo wakati wa mechi ya mchezo wa mpira wa kikapu kati ya timu ya Nigeria na Lithuania siku ya Jumanne.

Muendesha mashitaka katika kesi hiyo aliiambia mahakama ya Stratford mashariki mwa London kunakofanyikia michezo ya Olympic, kuwa mtuhumiwa alitoa maneno ya kejeli za kibaguzi baada ya kusikika akisema kuwa, kulikuwa na kelele za mtindo wa nyani wakati timu ya Nigeria ilipokuwa ikatawala kushika mpira wakati wa mechi hiyo.