Shirika la msaada wa matibabu, MSF, linasema kuwa ugonjwa unaouwa wa virusi vya Ebola, uliozuka Uganda, unaonesha kuwa umedhibitiwa.
Akizungumza na BBC, afisa mmoja wa MSF anayeshghulika na magonjwa yanayoambukiza, Dr Paul Roddy, alisema kifo cha mwisho kilichosababishwa na Ebola kilitokea siku 11 zilizopita.
Lakini alionya kwamba iwapo kuna virusi eneo fulani ambavyo bado havikushughulikiwa, ugonjwa unaweza kujitokeza tena.
Alisema imethibitishwa kuwa vifo 19 vilitokana na ugonjwa uliotokea kwenye mji wa Kagadi.
Dr Roddy alisema inawezekana virusi hivo vilitokana na popo, ambao pengine waliwaambukiza nyani - nyama ya nyani huliwa na wawindaji.