Gu mke wa Bo Xilai, mwanasiasa wa Uchina
Mke wa mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa nchini Uchina Bo Xilai amepatiwa hukumu ya kifo ambayo badala yake atatumikia kifungo gerezani kwa mauaji ya mfanyabiashara wa Uingereza Neil Heywood.
Gu Kailai hakupinga mashitaka dhidi yake katika kesi hiyo iliyochukua siku moja ya kumuua kwa kutumia sumu Bwana Heywood mwezi Novemba mwaka 2011.
Hukumu za kifo mara nyingi huwa ni kifungo cha maisha nchini Uchina.
Bwana Bo, kiongozi mkuu wa zamani wa chama mjini Chongqing, alikuwa akitegemewa kugombea nafasi ya uongozi wa juu kabisa baadaye mwaka huu.
Lakini hajaonekana hadharani tokea kuanza kwa uchunguzi dhidi ya mkewe Gu kutangazwa kuanza.
Msaidizi wa Gu, Zhang Xiaojun, alihukumiwa kifungo cha miaka tisa kwa ushiriki wake katika mauaji hayo.