Na Waandishi Wetu
MWANAMUZIKI aliye juu kuliko wote kwa sasa kwenye Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond Platinumz’ yamemkuta baada ya kuugua ghafla na kulazwa huku hali yake ikielezwa kuwa siyo nzuri ikiwa ni siku chache tangu amchane baba’ke Abdul Juma, Ijumaa linafunguka ripoti kamili.
AKIMBIZWA HOSPITALINI
Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni ndugu wa karibu wa staa huyo, Jumanne ya Julai 31, mwaka huu, Diamond alikimbizwa Hospitali ya Heameda Medical Clinic iliyopo Upanga jijini Dar akisumbuliwa na ugonjwa uliomshambulia sehemu ya kifua.
CHANZO CHATIRIRIKA
“Naongea na Ijumaa? Kwa taarifa yenu dogo (Diamond) hali yake si nzuri leo (Jumanne wiki hii) na hivi ninavyowaambia tuko hospitali anafanyiwa uchunguzi,” alisema ndugu huyo wa Diamond kisha akakata simu ndipo waandishi wetu wakaingia mzigoni na kunyaka mchongo kamili.
Baada ya chanzo kuingia mitini, Ijumaa lilianza kumfuatilia Diamond hadi likampata na kuzungumza naye akiwa hoi.
Kwanza ‘kichaa’ huyo wa muziki alikiri kuumwa ghafla na kukimbizwa hospitali kisha akaendelea kudadavua kilichomsibu
.

TUMSIKIE DIAMOND
“Diamond hatunaye tena....hiyo ndiyo ingekuwa kichwa cha habari kwenye ‘midia’ na watu wengi kwenye social networks (mitandao ya kijamii) na simu zao.
“Kiukweli hali yangu ilikuwa ni mbaya sana, nilizidiwa na homa kali ya ghafla iliyosababishwa na kifua kilichonisumbua kwa takribani wiki mbili mfululizo.
“Namshukuru Mungu baada ya vipimo vyote iligundulika ni kifua cha kawaida tu ila kilisababishwa na tour (ziara) nyingi nilizozifanya mfululizo bila mapumziko.
LAKINI ANAENDELEAJE?
“Kwa sasa hali yangu si mbaya sana...nawashukuru wote waliokuwa wakiniombea,” alifunguka Diamond.
HOFU YATANDA
Diamond aliendelea kufunguka kuwa hofu ilitanda kuhusu hatima yake ndiyo maana akawaambia madaktari wampime kila kitu ikiwemo Virusi Vya Ukimwi (VVU).
“Nilichanganyikiwa kwani sikuelewa ni nini hasa kilichonitokea hadi mawazo yangu yakaenda mbali na kuwaza labda nimeukwaa ndipo nilipowaambia madaktari cha kwanza kunipima ni huu ugonjwa wa kisasa,” Alisema Diamond.
WEMA NAYE GONJWAGONJWA
Katika hali ya kushangaza, Ijumaa lilipozungumza na mpenzi wa Diamond kwa sasa, Wema Isaac Sepetu, naye alikiri kuwa mgonjwamgonjwa (hakutaja ugonjwa ndiyo maana alishindwa kwenda hospitalini kumhudumia ‘hubby’ wake huyo.