Na Imelda Mtema
MCHEZA sinema wa Bongo aliye nyuma ya nondo katika Gereza la Segerea, jijini Dar es Salaama kwa madai ya kuhusika na kifo cha Msanii Steven Kanumba, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema kuwa amepamisi sana uraiani.
Akizungumza na mwandishi wetu Agosti 13, mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambako kesi yake inaendelea kutajwa, Lulu alisema amemisi vitu vingi vya uraiani, ikiwemo mitaa ya Sinza na Kinondoni alikozoea kwenda kujiachia, pia anawakumbuka sana mashosti wake akina Diana Kimaro ‘Pacha wa Lulu’.
“Nimekumisi sasa… (anataja jina la mwandishi), pia nimewamisi watu wote huko uraiani, nimewamisi mashosti wangu jamani, nimemisi sehemu nilizokuwa napenda kutembelea,“ alisema Lulu.
Lulu akionesha uso wa uchangamfu alisema anafurahi sana anapoona watu wanaofika mahakamani hapo ni baadhi ya marafiki zake na ndugu.
“Ukikaa kule (gerezani) unawakumbuka watu wengi, sasa ukija hapa (mahakamani) unapowaona watu mbalimbali unaowafahamu kidogo unafarijika, unakuwa mwenye amani siku hiyo,” alisema Lulu.