Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Sazi Salula akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na mkutano huo
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Magessa Mulongo akiongelea mkutano huo mbele ya waandishi wa habari.
 
Picha na habari na
Woinde Shizza,Arusha

 MAWAZIRI wa nchi za Afrika wanatarajia kuwasili jijini Arusha kwa ajili ya mkutano wa 14 wa mazingira utakaofanyika jijini hapa kuanzia september 10 hadi 14 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi wa mazingira katika nchi za afrika ambeye ndie mratibu wa mkutano huo Bw. Mounkaila Goumandakoye alisema kuwa mkutano huo utashirikisha mawaziri wa nchi za Afrika ambapo watazungumzia utunzaji wa mazingira na jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyoikumba nchi za afrika.
Alisema kuwa mkutano huu unashirikisha zaidi ya watu 3000 ambao wote watakuja kuzungumzia swala hilo .
Katibu mkuu wa ofisi ya Makamu wa Rais mazingira Mhe. Sazi Salula alisema kuwa mkutano huu ni wa 14 na kwa mwaka huu nchi yetu imepewa heshima pekee ya kuwa mwenyeji wa mkutano huu ambapo alibainisha kuwa waziri wa mazingira ndie ambaye atakuwa mwenyeji wa wageni hao ambapo alisema kuwa pia atakuwa mwenyekiti wa mkutano huu.
Salula alibainisha kuwa Tanzania imepewa heshima ya kipekee kwani imepangiwa kuwa mwenyeji wa mkutano huu kwa miaka miwili mfululizo yaani mwaka huu wa 2012 pamoja na mwaka 2013.