Serikali za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi
za Elimu ya Juu Zanzibar zatoa azimio la kuwataka wanafunzi na vijana kuweka
mbele maslahi ya nchi kwa kuelimishana na kuhamasishana juu ya haja ya
kuirudisha Jamhuri ya Watu Wazanzibar na Muungano wa mkataba ili Zanzibar iwe na
mamlaka kamili.
Azimio hilo lilitolewa kwenye kongamano
lililofanyika juzi Jumamosi katika ukumbi a Salama Hall Bwawani. Zaidi ya
wanafunzi mia tano na ishirini walihudhuria kongamano hilo pamoja na kuwa
lilifanyika katika kipindi cha matayarisho ya mwisho ya eid.
Hii ni kuonesha ni kiasi gani wanafunzi wa vyuo
na vijana wameamka katika harakati za kuitetea nchi yao na kutaka Zanzibar iliyo
na mamlaka kamili na muungano wa mkataba.
Watoa mada katika kongamano hilo alikuwa ni
pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ndugu Ibrahim Mzee, Mhadhiri kutoka SUZA
ndugu Ali Vuai, Mtaalam wa mambo ya Uchumi ndugu Mselem Khamis Mselem. Pia Bi
Naila Jidawi nae alieleza machache.
Nae Mwakilishi wa Kiembesamaki Mh. Mansor
Yussuf Himid alipoingia kwenye ukumbi huyo kama mualikwa alishangiriwa na
wanafunzi na vijana kwa makofi na hoihoi na kuombwa azungumze japo machache na
wanafunzi hao walionekana kuwa na hamu ya kumsikia Mwakilishi huyo waliozoea
kumuona akinguruma barazani kupitia vyombo vya habari.
Pamoja na michango mingi ya wanafunzi na
vijana hao, nao walimpongeza Mwakilishi Mansour pamoja na Wawailishi wengine
walioonesha moyo na ujasiri kama wake wa kuitetea Zanzibar na kuahidi kuwa
wataendelea kuwaunga mkono na wako pamoja nao bega kwa bega.
Walisema kuwa zama za kutishana zimepitwa na
wakati. Huu ni wakati wa hoja hasa wakizingatia wao ni vijana wasomi wa
Zanzibar.
Azimio pia liliitaka Tume ya Mabadiliko ya
Katiba izingatie misingi ya kuyaheshimu maoni ya wananchi juu ya aina gani ya
muungano wautakao.
Azimio hilo pia lililaani vikali vitisho
vinavyotolewa na baadhi ya wanasiasa wachache wenye kulinda maslahi yao binafsi
badala ya yale ya waanchi na taifa kwa ujumla.
Katika wageni waalikwa maamiri wa jumuiya ya
uamsho na mihadhara ya kiiskam nao walihudhuria ambapo waliwakilishwa na Amir
Mselem
0 Comments