Serikali ya Uingereza inatayarisha msaada wa dharura kwa ajili ya Sierra Leone, ambako kipindu-pindu kimeuwa watu zaidi ya 200.

Uingereza inataraji kuwapatia watu maji masafi na kujenga mitaro kwa watu kama milioni mbili.

Uingereza imeanza kusafirisha kwa ndege zana za matibabu na wafanyakazi hadi Sierra Leone.

Watu zaidi ya 12,000 wameambukizwa ugonjwa huo mwaka huu.