Serikali ya Tanzania inasema meli za mafuta 36 za Iran zimesajiliwa tena nchini
Tanzania, ili kujaribu kuhepa vikwazo dhidi ya Iran vilivowekwa na Marekani na
Umoja wa Ulaya.
Uchunguzi uliofaywa na serikali ya Tanzania, ambao ulionekana na shirika la
habari la Reuters, unaonesha kuwa serikali haikujua lolote kuhusu shughuli hizo
za kuzipatia meli za mafuta za Iran bendera ya Tanzania - shughuli iliyokuwa
ikifanywa na wakala alioko Dubai.Mafuta ya Iran yamewekewa vikwazo, ili kuishawishi Iran iache mradi wake wa nuklia.
Tanzania imeacha kuagiza mafuta kutoka Iran.
Uchunguzi ulifanywa na serikali ya Tanzania, baada ya mbunge mmoja wa Marekani, Howard Berman, mwenyekiti wa kamati ya Congress ya maswala ya nchi za nje, kueleza wasiwasi wake juu ya meli hizo za Iran kupatiwa bendera ya Tanzania.
Tanzania sasa inasema itafuta usajili wa meli hizo.
0 Comments