Stori: Sifael Paul na Vyanzo vya kimataifa
NDOA ya Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Morgan Richard Tsvangirai (60) aliyofunga Septemba 15, mwaka huu na mchumba’ke, Elizabeth Macheka (35), (pichani) jijini Harare, inadaiwa kupigwa zengwe.
Kabla ya tukio hilo lililofana vilivyo, tayari wanawake wawili walikuwa wameibuka na kudai kuwa ndoa hiyo ni batili hivyo waliweka vizuizi vya kisheria kwa madai kuwa mmoja alikuwa tayari ni mkewe na mwingine ni mchumba’ke.
Kwa mujibu wa duru za kihabari, baada ya aliyekuwa mkewe, Susan Nyaradzo Tsvangirai kufariki kwenye ajali ya gari mwaka 2009, kiongozi huyo wa chama cha siasa cha Movement for Democratic Change ĐTsvangirai (MDC-T), alimuoa mwanamke mwingine aitwaye Locardia Karimatsenga.
Siku chache kabla ya kufunga ndoa na Elizabeth, mwanamke mwingine, raia wa Afrika Kusini, Nosipho Regina Shilubane alikimbilia mahakamani kufungua kesi ya kusimamisha kufungwa kwa ndoa hiyo kwa madai kuwa Tsvangirai alikuwa amemchumbia na yeye ndiye aliyepaswa kuolewa.
Katika maelezo yake, Nosipho aliweka wazi kuwa yeye na Tsvangirai wamekuwa kwenye mapenzi mazito tangu 2009.
Hata hivyo, pamoja na vizingiti vyote, Tsvangirai aliwahi na kuifunga fasta ili kukwepa ‘stop order’ ya mahakama hivyo watu wakagonga mpunga na kuwapotezea waliokuwa wakiichokonoa ndoa hiyo isifungwe.