Godbless Lema akiwasili viwanja vya Mahakama Kuu Arusha kusikiliza rufaa yake mapema leo asubuhi.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Arusha waliofika eneo la Mahakama Kuu kusikiliza rufaa hiyo.Shauri lililofunguliwa na aliekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaaa nchini kupinga kuenguliwa kwake kuwa mbunge limeahirishwa hadi tarehe 2 mwezi ujao litakaposikilizwa tena.
Mapema asubuhi ya leo mamia ya wafuasi wa Chadema walijitokeza katika eneo la Mahakama Kuu kusikiliza rufaa hiyo ambayo ilisikilizwa kwa muda mrefu kiasi kabla ya kuahirishwa.
Taarifa za awali kutoka mahakamani hapo kabla ya kusikilizwa kwa shauri hilo hii leo zilieleza kuwa tayari mawakili wa pande zote mbili walishaandika barua ya kuomba kusogezwa mbele kwa shauri hilo hadi Oktoba 2, mwaka huu, kufuatia mawakili, Tundu Lissu, anayemtetea Lema na kaka yake, Alute Mughwai, anayewatetea walalamikaji, kufiwa na baba yao mzazi.
Imeelezwa kuwa, upande wa walalamikaji wameweka mapingamizi fulani ambayo jopo la majaji litayapitia hiyo tarehe 2 oktoba. Taarifa nyingine ambayo haijaweza kuthibitishwa na Blog hii zinaeleza kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa hukumu ya rufaa hii kusomwa Dar es Salaam...
KUSOMA ZAIDI BONYEZA HAPA