Tume ya Umoja wa mataifa inayochunguza ukiukwaji wa haki za
binadamu nchini Syria, imekusanya majina ya washukiwa vitendo vya uhalifu wa
kivita nchini humo.
Wachunguzi wa tume hiyo wanawashutumu wanajeshi wa serikali kwa kuhusika
katika uhalifu wa kivita.
Ripoti hiyo ni mojawapo ya ripoti zinazoikosoa zaidi serikali ya Syria kuwahi
kupokelewa na Umoja wa Mataifa.
Mkuu wa tume hiyo Paulo Pinheiro, alisema kuwa lina ushahidi wa kutosha
kuhusiana na madai hayo.
Alisema kuwa ana orodha ya majina ya washukiwa wakuu wa uhalifu wa kivita na
kutaka Umoja wa mataifa kuwasilisha kesi ya uhalifu wa kivita dhidi ya Syria kwa
Umoja wa Mataifa.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-Moon ametoa wito kwa baraza hilo la
haki za binamu kuchukua hatua.
Wakati huohuo, shirika la kutetea haki za kibinadamu la Huma Rights Watch,
limesema kuwa lina ushahidi wa kuthibitisha kuwa waasi nchini syria wamewatesa
mateka mbali na kuwauwa wengine.
Shirika hilo ilikusanya ushahidi mwezi jana wa mauaji na mateso dhidi ya
mateka yanayotekelezwa na upinzani katika mji wa Allepo na maeneo jirani .
Ripoti ya shirika hilo inalenga madai ya mauaji ya watu wanne wa familia moja
na vuguvugu la Free Syrian Army.
Human Rights Watch linasema kasi ambapo watu hao waliuwawa inafanya madai ya
upinzani kuwa walitendewa haki kuwa urongo mtupu |
0 Comments