OGANAIZESHENI YA NGUMI ZA KULIPWA TANZANIA [TPBO]
INAWAPA TAARIFA KWAMBA IFIKAPO TAREHE 27-10-2012 KUTAFANYIKA TAMASHA KUBWA LA MASUMBWI YA KULIPWA YATAKAYOWASHIRIKISHA MABONDIA KUTOKA KENYA NA TANZANIA .
TAMASHA HLI LINAANDALIWA NA REDIO SAFARI CHINI A MKURUGENZI WAKE NDG HARUN MTAFAKARI NA LINASIMAMIWA NA TPBO AMBAYO TAYARI IMESHATOWA KIBALI CHA MAPAMBANO HAYO

BONDIA MAARUFU NCHINI NA DUNIANI KOTE MBWANA MATUMLA ATAPAMBANA NA BONDIA ABDUL NOOR KUTOKA KENYA /
KATIKA UZITO WA SUPER BANTAM kilo gramms 55.8 WATAPIGANA RAUNDI 8

NA BONDIA MKONGWE NA BINGWA WA DUNIA KATIKA MATAJI MBALI MBALI RASHID MATUMLA ATAPAMBANA NA BONDIA KUTOKA KENYA PATRIC AMOTE KWENYE UZITO WA SURPER MIDDLE KILOGRAMMS 76 NA WATAPIGANA RAUNDI 8

TAMASHA HILO PIA LITAWASHIRIKISHA MABONDIA KUTOKA BLACK MAMBA YA MTWARA WAO WATAPAMBANA NA MABONDIA KUTOKA DAR-ES-SALAAM

MAANDALIZI YA TAMASHA HILI YANAENDELEA VYEMA NA MABONDIA WOTE WAMESHASAINISHWA MIKATABA YA MAPAMBANO YAO NA WANAJIFUWA VILIVYO.


TPNO INAFURAHISHWA SANA NA JINSI MAPROMOTA WANAVYOJITOKEZA SEHEMU MBALIMBALI NCHINI NA KUWAANDALIA MABONDIA MAPAMBANO ILI WAJIPATIE RIZIKI ZA KUJIKIMU KIMAISHA NA TPBO INAWATAKA WALE MABONDIA AMBAO HUCHUKUWA MALIPO YA AWALI KWA MAPROMOTA NA KISHA KUINGIA MITINI BILA KUFIKA ULINGONI ,WAACHE MARA MOJA MTINDO HUO KWANI ITAWAKATISHA TAMAA MAPROMOTA NA KUUKIMBIA KABISA MCHEZO WA NGUMI NA ITAPELEKEA MABONDIA KUJIINGIZA KATIKA VTTENDO VYA UHALIFU KWA KUKOSA HELA ZA MATUMIZI, VITENDO AMBAVYO TPBO INAVILAANI MARA ZOTE. NA TPBO DAIMA HAITAKUWA TAYARI KUFANYA KAZI NA MABONDIA WENYE TABIA HIZO ZA KITAPELI.


IMELETWA KWENU NAMI

YASSIN ABDALLAH -USTAADH

RAIS TPBO