Mkuu wa bunge la Libya anasema kuwa watu kama 50 wamekamatwa kwa kuhusika na
mauaji ya balozi wa Marekani mjini Benghazi juma lilopita.Mohammed Megaryef, kiongozi wa bunge, alisema hakuna shaka kuwa shambulio
hilo lilikuwa limepangwa na siyo tu la kulipiza kisasi kwa filamu ya Marekani
iliyokejeli Uislamu.
Akizungumza na shirika la habari la Canada, CBS, Bwana Megaryef alisema
anaamini wageni wenye uhusiano na Al-Qaeda walihusika.
Balozi wa Marekani, Chris Stevens, na Wamarekani wengine watatu, waliuwawa
wakati guruneti lilipopiga ubalozi mdogo wa Marekani mjini Benghazi na kuwaka
moto. |
0 Comments