Stori:Gladness Mallya MKURUGENZI wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo,’ Ally Choki (picha ndogo) amesema hakuna kitu kinachompa wakati mgumu kwa sasa kama bifu lake na Bosi wa African Stars ‘Twanga Pepeta,’ Asha Baraka.Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni jijini Dar, Choki alisema: “Hili bifu linaniweka pagumu, huwa najiuliza nikifa leo, Asha atabaki anajilaumu au atafurahia? Lazima atajuta ni kwa nini hatukumaliza tofauti zetu.”Choki anakabiliwa na tuhuma ya kuingia mitini na gari la Asha Baraka ambapo kesi ya msingi bado inazidi kurindima katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, Dar ikiendeshwa na Mheshimiwa Sanga, hukumu yake inatarajiwa kutolewa Novemba 28, mwaka huu. |
0 Comments