Luteni Kanali Sagir Musa anasema kuwa washukiwa wanne wa Boko
Haram walikamatwa katika msako uliofanywa usiku kucha.
Jeshi nchini Nigeria limesema limewaua washukiwa 24 wa kundi
haramu la Boko Haram mjini Maiduguri Kaskazini mwa Nigeria.
Wanajeshi waliziba barabara kuu mjini humo baada ya kutokea msururu wa
milipuko na milio ya risasi usiku kucha.
Kwa mujibu wa Jeshi, Boko Haram walishambulia kambi za jeshi.
Mwalimu wa shule ya msingi aliuawa huku mnara wa kupeperushia matangazo ya
redio ukichomwa.
Mapema mwezi huu, walioshuhudia makabiliano kati ya jeshi na washukiwa wa
Boko Haram, walisema kuwa wanajeshi waliwapiga risasi raia 30 baada ya
shambulizi la bomu dhidi ya kambi ya jeshi mjini Maiduguri.
Katika tukio la hivi karibuni, ripoti zinasema kuwa wanajeshi walifunga
karibu kila barabara mjini wakati mashambulizi yalipoanza Jumatatu adhuhuri na
kuendelea hadi masaa ya usiku.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema kuwa mapema Jumatatu mtu aliyekuwa
amejihami alishambulia kwa risasi polisi aliyekuwa anashika doria mjini humo
karibu na kizuizi barabarani.
Mapema mwezi huu, wanajeshi mjini Maiduguri, waliwashambulia watu baada ya
kutokea shambuli la bomu na kumuua mwanajeshi mmoja.
Walichoma maduka ya watu pamoja na nyumba.
Jeshi lilikana mauaji hayo ingawa waandishi wa habari wanasema kuwa lilitoa
maelezo ya kina kuhusu kilichotokea
Mashambulizi Kaskazni mwa Nigeria ambayo yamefanywa na Boko Haram
yamesababisha vifo vya watu 1,400 tangu mwaka 2010.
Maiduguri ndiyo ngome kuu ya Boko Haram ambao wanapigania kile wanachosema ni
sheria za kiisilamu kutumika nchini humo. |
0 Comments