Waasi wa M23 wanaosemekana kuungwa mkono na Uganda pamoja na
Rwanda
Uganda inatishia kujiondoa katika mazungumzo ya kuleta amani
katika nchi kadhaa barani Afrika.
Tisho hilo linafuatIa ripoti ya Umoja wa mataifa iliyokashifu Uganda kwa
madai ya kuunga mkono makundi ya waasi katika Jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo.
Waziri wa serikali , Asuman Kiyingi, alisema kuwa dhana kuwa Uganda inaunga
mkono waasi wa M23 katika DRC wakati ikiwa mpatanishi mkuu katika mazungumzo ya
amani ni njama ya kuidhalilisha na kuiharibia sifa nchi hiyo.
Aliongeza kuwa , ikiwa madai hayo hayataondolewa dhidi yake pamoja na juhudi
za nchi hiyo kukosa kutambulika, serikali itaondoa wapatanishi wake kwenye
mazungumzo ya amani.
Amesema pia vikosi vya nchi hiyo vilivyo nchini Somalia na Jamuhuri ya Afrika
ya Kati, pia vitaondolewa.
Vikosi hivyo vinaungwa mkono na Umoja wa Mataifa hatika harakati zao dhidi ya
waasi na wanamgambo. |
0 Comments