Kumetokea mlipuko mkubwa katika kampuni ya kutengeneza silaha katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum.
Mlipuko huo ulisababisha moto mkubwa na milipuko zaidi ilifuatia wakati wazima moto walifika kujaribu kuudhibiti moto huo, uliozuka kutoka kampuni hiyo ya Yarmouk .
Gaavana wa eneo hilo (Abdul Rahman Al-Khider Rahman) amesema watu kadha wamepelekwa hospitalini baada ya kuvuta moshi lakini hakuna aliyefariki.
Amesema kuwa mlipuko wa kwanza ulitokea katika hifadhi ya silaha na bado chanzo chake kinachunguzwa. Vifaa vingi vya kijeshi viko karibu na kampuni hiyo.