Maarohanye aliwagonga wanafunzi kwa gari kake mjini Soweto mwaka 2010 na
kuwaua wanafunzi wanne huku akiwajeruhi wengine wengi.
Jamaa za watoto waliofariki, walilia wakati jaji akitoa uamuzi wake.
Maarohanye alikuwa mmoja wa wanamuziki wenye sifa sana nchini Afrika Kusini
ingawa baada ya kitendo chake umaarufu wake ukaanza kudidimia.
''Tunawapongeza sana viongozi wa mashtaka kwa kuchukua msimamo wa kuwapata na
hatia ya mauaji madereva walioendesha magari wakiwa walevi,'' alisema afisaa
katika wizara ya sheria.
Mshtakiwa mwenza wa Maarohanye, Themba Tshabalala, pia alihukumiwa kwa kosa
la mauaji.
Walikuwa wanatumia madawa ya kulevya wakati magari yao yalipowagonga
wanafunzi. Hata hivyo walikana mashtaka dhidi yao.
Wawili hao walikuwa nje kwa dhamana tangu mwaka 2010 mwezi Machi, uamuzi
ambao ulisababisha maandamano makubwa ya wanafunzi waliotaka wawili hao kufungwa
jela.
Hakimu Nemavhidi, alibatilisha uamuzi wa kuwaachilia kwa dhamana na kuwaweka
rumande hadi hukumu itakapotolewa mwezi Novemba tarehe 30 |
0 Comments