Wanawake wamekuwa wakinyimwa nafasi ya kurithi Botswana
Mahakama kuu nchini Botswana imebatilisha sheria ya kitamaduni
ambayo iliwazuia wanawake kurithi mali nyumbani.
Mahakama imesema kuwa kanuni hiyo ya kitamaduni inakiuka sheria ya katiba
inayosisitiza usawa kwa wanaume na wanawake.
Edith Mmusi na dadake zake watatu walilazimika kwenda mahakamani baada ya
mpwa wao kusema kuwa yeye ndiye mmiliki wa nyumba yao.
Duru zinasema kuwa wanawake hawaruhusiwi kurithi mali katika jamii nyingi za
kiafrika ingawa katika baadhi ya nchi sheria hizo sasa zinaharamishwa.
Mwandishi wa BBC mjini Gaborone, anasema kuwa uamuzi wa jaji Key Dingake,
sasa inaileta katika safu moja sheria ya utamaduni na katiba ya nchi.
Alisema kuwa lazima pawepo usawa kati ya wanawake na wanaume kuhusiana na
swala urithi.
Mmoja wa madada hao waliofika katika mahakama kupinga sheria za kitamaduni ,
alijawa na furaha isiyo na kifani.
"ni siku nzuri sana kwetu'' alisema bi Mmusi
Uamuzi wa leo unafikisha kileleni kesi ambayo imekuwa ikiendelea kwa miaka
mitano ambayo yeye na madada zake walifikisha mahakamani.
Mussi walienda mwanzo katika mahakama za kitamaduni kupinga hatua ya mpwa wao
mnamo mwaka 2007.
Lakini walishindwa katika kesi hiyo mara mbili ndiposa wakaamua kwenda katika
mahakama ya kiraia. |
0 Comments