Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akisaini kitabu cha wageni jana katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, wakati akiwa katika ziara ya siku mbili Mkoani humo.
Mhe. Waziri Membe akifafanua kuhusu mgogoro wa Mpaka wa Ziwa Nyasa kati ya Tanzania na Malawi mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama chini ya Uenyekiti wa Mhe. Abbas Kandoro, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.
Mhe. Waziri Membe na msafara wake wakiwa wamesimama kwenye mpaka wa Mto Songwe.
Waziri Membe akiangalia Mto Songwe, huku akitafakari mpaka kwa vile hapo aliposimama kwa ufupi ni nchini Malawi ambapo wananchi wa pande zote wanapishana kuendelea na shughuli zao za kawaida (angalia alama ya tundu lililoko chini ya fensi – kulia).
Mhe. Waziri Membe akiongea na Wajumbe wa msafara wake akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Abbas Kandoro (mwenye shati jeupe mbele ya Waziri), Balozi Irene Kasyanju (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria kwenye Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Balozi Dkt. Mohamed Maundi (kushoto), Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia – Kurasini. (Picha hii na Mbaraka Islam)
Makazi ya wananchi wa Malawi kando ya Mto Songwe ambapo mmoja wa wananchi anaonekana akifua nguo (pichani – upande wa kushoto; ng’ando ya mpaka kwa upande wa Malawi) wakati wengine (kulia) wanaonekana wakiendelea na shughuli zao za kawaida huku wakiwa tayari wamevuka ng’ando ya mpaka kwa upande wa Tanzania.(Picha, maelezo na Tagie Daisy Mwakawago).