Mashabiki wa timu ya Simba wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali, Makao Makuu ya klabu hiyo Mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam jana, kuonesha hasira zao baada ya timu hiyo kusuasua katika michezo yake ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, ambayo ilifungwa bao 2-0 na Mtibwa Sugar, kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.