Polisi nchini Uganda wamewazuia wanaharakati wa kupinga ufisadi kufanya maandano katika barabara za mji mkuu wa nchi hiyo, Kampala.
Karibu wanaharakati 300 waliokuwa wamevalia nguo nyeusi walilazimika kukatiza maandamano yao baada ya polisi waliojihami kwa silaha kuziba barabara zote.
Mwanahabari wa BBC amesema maandamano hayo yamefanyika kufuatia ufichuzi katika vyombo vya habari kuhusu visa kadhaa vya ufisadi ikiwemo madia kwamba zaidi ya dola milioni 15 za misaada ya kigeni zimeishia mifukoni mwa wakuu fulani serikalini.