Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Korea nchini Tanzania, IL Chung.
Pia, Makamu wa Rais amezungumza na mgeni wake huyo juu ya kuangalia uwezekano wa Korea kuisaidia Tanzania katika suala zima la utunzaji wa mazingira na matumizi ya nishati zenye madhara chanya kwa mazingira, Mheshimiwa Makamu wa Rais alieleza kuwa hivi sasa Tanzania ina tatizo kubwa la mazingira kutokana na uharibifu mkubwa unaotokana na matumizi ya miti kama nishati muhimu kwa wananchi hasa wa vijijini.
0 Comments