Michael Schumacher anajiandaa kushiriki mashindano yake ya mwisho kabisa katika taaluma yake
Schumacher ataendesha gari la Formula One kwa mara ya mwisho Jumapili hii katika mkondo wa Brazil Grand Prix. Schumacher anashikilia rekodi karibu zote za Formula One, ikiwa ni pamoja na ushindi 91 wa Grand Prix na kupata nafasi za kwanza 68 pamoja na mataji saba ya ubingwa wa F1 akiwa na timu za Benetton na Ferrari.
Mkufunzi wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Loew anasema Schumacher ni jina maarufu kispoti kote ulimwenguni siyo tu nyumbani kwao Ujerumani. Mafanikio yake katika F1 yanajieleza yenyewe na kamwe hayatasahaulika.
Familia ya F1 imemsifu dereva huyo huku Kiongozi wa Ferrari Stefano Domenicali akisema jina la Schumacher limehusishwa na takribani nusu ya ushindi wa timu yake na atasalia mioyoni mwa familia ya Ferrari. Rais wa Mercedes Ross Brawn ambaye amewahi kufanya kazi na Schumacher kwa muda mwingi wa taalum yake amesema mbio za kesho nchini Brazil zitakuwa na huzuni kwa kila mtu katika kikosi chao