Baraza la sanaa la Taifa limeteuwa majina matatu kati ya sita ya majaji yaliopendekezwa na waandaji wa shindano la kumsaka mwanamitindo wa mwaka mwenye sifa za kipekee.
Uteuzi huo wa wabunfu Asia Idarous khamsini,Gymkhana Hilall (paka wear) na Martin Kadinda umefanyika mwishoni mwa wiki hii baada ya baraza la sanaa la Taifa (Basata) kupitia wasifu wao na kuridhika wawe waamuzi rasmi wa shindano la Unique model 2012.
Kinyang’anyiro cha kumsaka mwanamitindo huyo wa mwaka kinajumuisha washiriki kumi na mbili katika jukwaa moja ambapo fainali hizi zitafanyika tarehe 28 desemba katika ukumbi wa maraha New Maisha club ulioko Oysterbay jijini Dar.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mratibu wa shindano hilo Methuselah Magese amesema kuwa maandalizi ya shindano hilo yako vizuri sana na washiriki wamenorewa kiasi cha kutosha imebaki ni kazi ya umatiwa wapenzi wa mambo ya mitindo kujitokeza kwa wingi kushuhudia nani atachukua taji siku ya ijumaa.
Shindano la unique model litapambwa na burudani toka bendi ya mashujaa ikiongozwa na rapa maarufu Chalz Baba ikiambatana na ngoma za asili toka kwa Costa Siboka na utambulisho wa msanii mkali wa bongo flava B-shop kwa mara kwanza atatoa burudani ambayo haijawahi kutokea.
Magese aliongeza kuwa mbali ya burudani kutakuwa na zulia jekundu(Red carpet) kwa watu maarufu na watu waliopendeza zaidi siku hiyo ambapo kiingilio kitakuwa ni Tshs 15,000 tu kiingilio ambacho hakitengi tabaka la watu flani katika jamii.i
|
0 Comments