Alisema mashtaka yaliyoahirishwa kutokana na wahusika kuhitaji ushauri wa kisheria ni madaktari wanne na mashtaka yasiyosikilizwa kutokana na wahusika kutofika walipoitwa na Baraza ni madaktari 22.
“Wizara inakamilisha taratibu za kinidhamu kwa mujibu wa Kanuni za Utumishi wa Umma kwa Madaktari wote waajiriwa ambao walipatikana na hatia mbele ya Baraza la Madaktari,”aliseleza Mwamaja na kuongeza
“Wizara pia imeridhia kuwapa madaktari waliokuwa katika mafunzo kwa vitendo fursa nyingine ya kuendelea na mafunzo hayo katika hospitali za Umma walizokuwepo kabla ya kuondolewa.”
Hata hivyo alisema fursa hiyo haitawahusu madaktari wote waliopewa adhabu za kusimamishwa na Baraza la Madaktari, hadi hapo watakapomaliza kutumikia adhabu zao.
Alisema kwa taarifa hiyo madaktari wote waliofutiwa mashtaka na wale waliopewa onyo na onyo kali wanatakiwa kuwasilisha kwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii barua kutoka kwa msajili wa Baraza la Madaktari ikithibitisha kurejeshewa usajili na kuruhusiwa kuendelea na mafunzo kwa vitendo.
Vile vile madaktari waajiriwa(Registrar) wanatakiwa pia kuripoti kwa Katibu Mkuu ili kupewa
barua zao kulingana na Adhabu walizopewa.
0 Comments