Maafisa wa serikali nchini Japan wameanza ukaguzi wa dharura kote nchini kuzuia kutokea ajali kama ya jana ambapo watu tisa waliuawa.
Waliuawa wakati njia ya chini ya kupitia magari inayounganisha mji wa Tokyo na Japan ya kati iliporomoka na kusababisha magari kukwama na moto kuzuka.
Ukaguzi uliofanywa miezi miwili iliyopita haukubainisha matatiozo yoyote na njia hiyo.
Serikali sasa imaemrisha ukaguzi wa kiwango cha juu wa kiasi ya njia nyengine ishirini za chini ya ardhi zenye umri na muundo sawa na njia ya Sasago.