Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara (kushoto) akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Massawe mara baada ya kumtembelea ofisini kwake jana mjini Bukoba. Waziri Dk. Mukangara yupo mkoani humo kwa ajili ya kuangalia jinsi fedha za mkopo kutoka mfuko wa vijana zilivyoweza kuwasaidia vijana kujikwamua kimaisha.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe alipomtembelea ofisini kwake jana mjini Bukoba. Waziri Dk. Mukangara yupo mkoani humo kwa ajili ya kuangalia jinsi fedha za mkopo kutoka mfuko wa vijana zilivyoweza kuwasaidia vijana kujikwamua kimaisha.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (kushoto ) akiongea na viongozi wa mkoa wa Kagera (hawapo pichani) jana mjini Bukoba jinsi Serikali inavyoangalia uwezekano wa kuongeza mkopo kwa SACCOS zinazolenga shughuli za maendeleo ya vijana kutoka shilingi milioni tano hadi kumi kutokana na mahitaji ya fedha hizo kuwa makubwa. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana James Kajugusi.
(Picha na Anna Nkinda – Maelezo)