Na Mwandishi Wetu
MASWALI matatu yamegubika ukaribu wa ‘ziro distensi’ kati ya Miss Tanzania 2006 ambaye pia ni staa wa filamu za Bongo, Wema Sepetu na mbunifu wa mavazi, Martin Kadinda, Ijumaa linashuka nayo.
Maswali hayo yameibuka kufuatia safari ya wawili hao hivi karibuni Johannesburg, Afrika Kusini ambapo Wema ndiye aliyelipia gharama zote kiasi cha Shilingi Milioni 6.
Madhumuni ya safari yanaonesha ni ‘sapraizi’ ya Wema kwa kijana huyo kwenda kupumzika baada ya kushinda tuzo ya mbunifu bora wa mavazi ya kiume Bongo.

Akiwapasha wadau wake kwa njia ya mtandao kuhusu safari hiyo, Kadinda aliandika:
“Sioni kama kuna haja ya kutoshukuru kwa binti huyu (Wema) mwenye roho ya kipekee.
“Usiku wa Tar 8, Desemba (2012) , nilipata tuzo ya kuwa mbunifu bora wa mavazi ya kiume Tanzania. Ni kitu kikubwa sana kwangu na sikujua kama Wema Sepetu ameguswa na ushindi wangu.
“Usiku huohuo aliniita nyumbani na kunikabidhi tiketi ya ndege pamoja na mambo mengine yote. Sikuamini na nikahisi kama nadanganywa hivi.
“Asubuhi siku iliyofuata Mark X (gari) nyeusi ilinifuata na kupelekwa moja kwa moja airport. Mpaka naingia ndani ya ndege ilikuwa kama masihara hivi.
“…bata lilikuwa ndefu. Nampenda sana Wema na ‘mtu’ wake, maana wao ndiyo walionilipia gharama zangu zote.”
SWALI LA KWANZA
Martin anakiri mwenyewe kwamba, kule Afrika Kusini alikuwa na Wema. Hata baadhi ya picha zake kwenye mtandao zinaonesha amepiga na mlimbwende huyo.
Nyingine walipiga wakiwa chumbani, kwani sinki la kuogea linaonekana wazi. Je, huyo ‘mtu’ wake Wema amemwamini nini Kadinda kwenda Sauzi na mpenzi wake?
SWALI LA PILI
Katika ‘posti’ yake, Kadinda haoneshi kama yeye alifikia chumba cha peke yake. Je, walilala chumba kimoja?
SWALI LA TATU
Ijumaa lilizungumza na baadhi ya mastaa ambao waliomba hifadhi ya majina yao na kuwauliza kama Kadinda ana demu. Asilimia 95 walisema hawajawahi kumwona na demu ingawa amekuwa akipiga picha na mastaa mbalimbali wa Bongo.
“Kadinda anapiga sana picha na sisi mastaa, lakini sijawahi kusikia ana demu wala kuoneshwa demu wake.” Hii ni nukuu ya staa mmoja kati ya waliohojiwa na gazeti hili.
Je, Kadinda hana demu? Wema kwa sababu na yeye alikuwepo katika safari hiyo, alipaswa kumkatia tiketi mpenzi wa Kadinda (kama yupo) ili kuondoa maswali. Wema na Kadinda hawakuweza kupatikana mara moja kujibu maswali hayo. Tunaendelea kuwatafuta.

(PICHA ZOTE KWA HISANI YA MVUTO KWANZA)