STAA wa filamu za Kibongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ amefariki dunia leo alfajiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu. Kwa mujibu wa Katibu wa chama cha waongoza Filamu Wilaya ya Ilala, Rajabu Amiri ni kwamba hivi karibuni Sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen!

Enzi za uhai wake marehemu Sajuki kulia akiwa na mkewe Wastara,Kila mmoja alimpenda sana mwenziwe,Maganga One Blog inatoa pole kwa familia nzima ya marehemu.pumzika kwa amani ndugu yetu Sajuki,ama hakika ulikuwa kipenzi chetu.