Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wanachama wa UVCCM wa vyuo vikuu mkoani Tabora waliomtembelea Ikulu ndogo mkoani humo usiku wa kuamkia leo. Pamoja na mambo mengine Rais Kikwete aliwataka vijana hao kuzingatia masomo kwa nguvu zao zote, akisisitiza kwamba elimu ni ufunguo wa maisha hivyo wasome kwa bidii ili nchi ipate wasomi waliobobea katika kila nyanja katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.