Bondia wa ngumi za kulipwa na bingwa wa IBF INTERCONTINETAL
Ramadhani shauri anategemea kupanda ulingoni kesho kuzipiga na Said
njechele wa iringa katika pambano la kirafiki la raundi nane katika
ukumbi wa D.I.D Hall uliopo mabibo mwasho.
Mratibu
wa pambano hilo Charles Christopher mzazi ameeleza kuwa maaandalizi
ya pambano yapo kamili na mabondia wote wapo katika hali nzuri ya
ushindani na wamepima wapo sawa kabisa kwa kuzipiga. Ambapo pia
kutakuwepo na mapambano mengi ya utangulizi na mabondia watakaosindikiza
pia wamepima chini ya usimamizi wa katibu mkuu wa TPBO bw Ibrahim
kamwe na docta john wapo sawa kwa kupambana.
Mabondia
watakaocheza utangulizi ni kama ifuatavyo HAMIS MOHAMED na HARUNA
MNYALUKOLO, PENDEZA SHOMARI atazipiga na MARTIN RICHARD, MBARUKU NASORO
na KARIMU RESPECT, DOTO MUSTAFA atakabiliana na SHOMARI MIURUNDI, huku
ISSA OMAR akizipiga na JUMA J KASHNDE.
Katibu
mkuu wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahim Kamwe ama bigright amethibisha
kuwa kanuni na taratibu za ngumi za kulipwa zimefuatwa na mabondia
wapo katika hali nzuri ya kupigana hiyo siku ya jumapili katika ukumbi
wa DID HALL mabibo mwisho kati ya bingwa wa IBF INTERCONTINENTAL
RAMADHANI SHAURI na SAID NJECHELE
|
0 Comments