Wizara ya Ulinzi ya Ufaransa inasema kuwa jeshi linaloongozwa na
Wafaransa limeuteka uwanja wa ndege wa mji wa Gao, ngome ya wapiganaji
ya Kiislamu kaskazini mwa Mali.Daraja muhimu piya wameiteka.
Mapigano yanaendelea.
Gao ni mmoja kati ya miji mikuu mitatu ya kaskazini mwa Mali iliyotekwa na wapiganaji mwaka jana.
Siku ya Ijumaa wanajeshi wa Mali na Ufaransa waliukomboa mji wa Hombor kilomita 160 kutoka Gao.
Umoja wa Afrika umesema unataka kuzidisha idadi
ya wanajeshi wa kuweka amani nchini Mali, na imeomba nchi zanachama
kujitolea kwa wanajeshi zaidi katika wiki zijazo.
Piya umeuomba Umoja wa Mataifa usaidie kuwasafirisha wanajeshi hao hadi Mali. |
0 Comments