Wagonjwa watano wa mwisho miongoni mwa 37 waliokwenda India kwa ajili ya matibabu ya moyo, wamerejea salama baada ya upasuaji.
Wagonjwa hao walipokelewa jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere na viongozi mbalimbali wa klabu ya Lions ya Dar es Salaam
(host) na wafadhili mbalimbali waliowezesha matibabu hayo.
Akizungumza kwa niaba ya Rais wa klabu ya Lions ya Dar es Salaam (host),
Lion Nimira Gangji, mratibu wa magonjwa ya moyo katika klabu hiyo, Lion
Dk. Rajni Kanabar, alisema wagonjwa hao walitibiwa katika hospitali ya
Narayana Hrudayalaya Heart Institute, iliyoko mji wa Bangalore
Alisema wagonjwa walisafiri kwenda kwenye matibabu kwa ufadhili wa Lions
Club of Dar es Salaam ( Host) kwa kushirikiana na Regency Medical
Centre, Wizara ya Afya ya Zanzibar, Satya Sai Society ya Dar es Salaam,
Tanzania, Narayana Hrudayalaya Heart Hospital na Fortis Escort Heart
Hospital, New Delhi.
Alisema wagonjwa hao walisafirishwa kwenda kutibiwa Novemba, mwaka jana
na Rais wa Lions Host aliwashukuru wasamaria wote waliojitolea kwa hali
na mali kuwagharamia wagonjwa hao.
Aliishukuru hospitali ya Regency, Wizara ya Afya ya Zanzibar ambayo
iligharamia matibabu ya watoto saba, hospitali ya Fortis Escots,
Narayana Hrudayalaya kwa kutoa punguzo na kufanya upasuaji kwa dola
2,500, Sri Satya Sai Society Tanzania kwa kutoa tiketi tisa za ndege,
Sanjeev Kapoor aliyetoa dola 1,000.
Aliwataja wengine kuwa Sanjeev Kapoor, ambaye kwa kushirikiana na Lions,
alifanikisha kuchangisha dola 23,000, Shivacom waliotoa dola 2,500 na
dola 1,500 kwa gharama za matangazo.
0 Comments