Waasi wa Syria
Muungano wa upinzani umesema kuwa utahudhuria mkutano wa kimataifa Roma baadaye wiki hii na kubatilisha uamuzi wa awali wa kuususia .
Kiongozi wa Muungabno wa kitaifa wa nchi hiyo , Moaz al-Khatib, amesema mabadiliko hayo yametokana na na msimamamo wa waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na mwenzake wa Uingereza William Hague kuahidi kuwa watatoa msaada maalum kwa Syria ili kuwaokoa wananchi wanaoteseka.
Muungano huo ulikuwa umekataa kuhudhuria mkutano na marafiki wa Syria ukilalamika kuwa dunia ilikuwa kimya wakati makombora yalirushwa Aleppo.
Mapema waziri wa mambo ya nje wa Syria alisema kuwa serikali ilikuwa radhi kuzungumuza na wapinzani na vile vile waasi wa silaha.

Mkutanao huo wa Roma wa marafiki wa Syria utazungumzia kuhusu ziara ya kwanza ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry.
Awali kulikuwa na wasiwasi baada ya upinzani kutishia kususia. Hata hivyo bwana Kerry alimpigia simu kiongozi wa upinzani, Moaz al-Khatib, na kumhakikishia kuwa ni sharti upinzani kuhusishwa.
Mwenzake wa Uingereza William Hague alisema kuwa kuna mipango ya kusaidia upinzani.
Bila shaka habari hizi hazitaifurahisha serikali ya Syria ambayo imekuwa ikipendekeza kuwe na mazungumzo ya mapatano lakini upinzani umekuwa ukisistiza Rais Asad na maafisa wake wakuu wasihudhurie mkutano huo.